Dkt. Msonde atolewa NECTA
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI (Elimu), akichukua nafasi ya Gerald Mweli, ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo.