Dereva aliyesababisha vifo vya watu 6 akamatwa
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linamshikilia dereva wa lori, aliyesababisha ajali na kupelekea vifo vya watu sita na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kuigonga Toyota Noah, katika eneo la Alkatani, Kata ya Sepeko, Tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo.