Kijana ajinyonga na kuacha ujumbe wa wapi azikwe
Kijana Idrisa Milundiko ambaye ni dereva bodaboda, amekutwa amejinyonga katika pori la Kasokola mkoani Katavi kwa kutumia mkanda wa suruali huku akiacha ujumbe uliosomeka “kaka mimi naenda kujinyonga kwani nina matatizo mengi na mwili wangu upelekwe kwa mjomba wangu aishiye Makanyagio”.