Wanafunzi wajisaidia vichakani, vyoo vyao vyatitia
Wanafunzi katika shule ya msingi Kasaba kata ya Kidahwe halmashauri ya wilaya ya Kigoma wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia msituni kufuatia shule hiyo kutokuwa na huduma ya vyoo tangu mwaka 2020 baada ya kutitia.

