Askari waliogeuza simu za wizi miradi kuchunguzwa
Jeshi la Polisi Tanzania limeanza uchunguzi dhidi ya askari wanaotumia fursa ya watu kuibiwa simu kuanza kuwaomba pesa ili wawasaidie kutafuta simu hizo na hatua kali kwa askari wanaohusika na utovu huo wa nidhamu zitachukuliwa.