Mdee ahoji barabara ya Makongo lini itakamilika
Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, ameihoji Wizara ya Ujenzi juu ya lini kipande cha barabara kutoka Makongo Juu hadi Chuo cha Ardhi kitakamilika kwani mkandarasi aliyepewa kujenga kipande hicho toka mwaka 2020 hadi sasa bado anasuasua.

