Mume ajiua kwa sumu baada ya mke wake kumkataa
Ginasa Petro (30) aliyekuwa mkazi wa kijiji cha Kayenze, kata ya Kafita wilaya ya Nyang'hwale, amejiua kwa kunywa sumu ya Panya baada ya mke wake Sarah Jeremia kukataa kurudi kuishi naye baada ya hapo awali kuondoka kutokana na mgogoro wa kimapenzi.

