Mourinho afungwa mchezo wa 8, Serie A
Kocha wa AS Roma ya Italia Jose Mourinho amefungwa mchezo wa 8 kwenye Ligi kuu nchini Italia Serie A' msimu huu wa 2022-23, baada ya kufungwa mabao 3-1 na AC Milan. Kipigo hicho kimeifanya Roma isalie nafasi ya 7 na alama zake 32 ikiwa ni tofauti ya alama 14 dhidi ya Vinara Inter Milan.

