Chelsea ni timu bora kuliko Spurs - Conte
Kocha wa Tottenham Antonio Conte amesema Chelsea walikuwa bora zaidi yao kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Ligi Carabao Cup mchezo ambao ulimalizaka kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Kocha huyo amesema kuwa anakazi kubwa ya kufanya ili kuboresha kikosi chake.

