Manula, Taddeo kuikosa Mbeya City leo
Mabingwa wa Tanzania bara Simba Sc wataikosa huduma ya golikipa wake namba moja Aishi Manula na kiungo mkabaji Taddeo Lwangwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya City, mchezo utakao chezwa Saa 1:00 Usiku uwanja wa Benjamini Mkapa.

