Aishi Manula
Wachezaji hao wawili wataukosa mchezo huu kwa sababu wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano kila mmoja, hii ikiwa ni kwa mujibu wa kanuni ambapo mchezaji akifikisha idadi ya kadi tatu za njano atatumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja na nakuwa mchezo wa ligi unaofata baada kutimiza idadi ya kadi hizi.
Simba ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 70 na wanawaarika Mbeya city ambao wapo nafasi ya 13 wakiwa na alama 36. Mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulichezwa Jijini Mbeya katika dimba la Sokoine na Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 bao ambalo lilifungwa na nahodha John Bocco na katika michezo mitano ya mwisho timu hizi kukutana Simba imeshinda michezo yote.
Mchezo mwingine wa Ligi leo utachezwa saa 10:00 Jioni uwanja wa Nelson Mandela ambapo Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Coastal Union ya Tanga.


