Italia imebadilika, yamuogopesha Luis Enrique
Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Euro 2020 inachezwa leo saa nne usiku ambapo Mabingwa mara tatu wa michuano hii timu ya Taifa ya Hispania watakuwa wakiminyana na mabingwa wa mwaka 1968 timu ya Taifa ya Italia, mchezo huu utachezwa katika dimba la Wembley .

