Rekodi zaibeba Chelsea mbele ya Real Madrid
Hatua ya Nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya inaanza kutimua vumbi hii leo kwa mchezo wa nusu fainali ya kwanza, ambapo Real Madrid ya Hispania watakuwa nyumbani katika dimba la Alfredo Di Stefano kuwaalika wa Chelsea ya England.