FC Porto kupindua meza au Chelsea kutamba?
Wababe wa nchini Ureno, Klabu ya FC Porto itajitupa dimbani saa 4:00 usiku wa leo tarehe 13 Aprili 2021 kukipiga dhidi ya matajiri wa jiji la London, klabu ya Chelsea kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.