Hatma ya Cavani, ipo mikononi mwake
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemsifu mshambuliaji wake Edinson Cavani kwa kiwango bora alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Tottenham na anaamini atamshawishi asalie klabu hapo, mkataba wa mshambuliaji huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu.