Kesi ya uhujumu uchumi kwa watu watatu Tarime
Watu watatu, Joseph Mseth, James Mwita na Chausiku Nyangambe wote wakazi wa Ronsoti kata ya Nyamisangura, Tarime mkoani Mara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi kilo 53.15.