"Na akili zangu timamu sikabidhi kitu kibaya"- RC
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, amekataa kukabidhi madawati 50 pamoja na meza 10 za walimu katika shule ya msingi Mtakanini iliyopo wilaya ya Namtumbo mkoani humo baada ya kukuta meza pamoja na madawati yakiwa mabovu na kuagiza yaende yakafanyiwe marekebisho.