Wananchi wagoma kufungiwa mita za maji
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kalela wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wametishia kutotumia maji yanayotolewa na mradi wa maji uliojengwa katika eneo hilo kama hatua ya kugomea kufungiwa mita kwa madai ya kuwa gharama za matumizi yake haziendani na kipato chao.