Mwanamke mjamzito, ajikuta hana ujauzito
Taharuki imeibuka kwa wakazi wa kitongoji cha Iyula A katika kata Iyula, wilayani Mbozi, baada ya mwanamke mmoja Mariam Mligo (19) anayedaiwa kuwa mjamzito wa miezi tisa, ujauzito wake kupotea katika mazingira tata muda mfupi baada ya kushikwa na uchungu.