Vyuo vya Afya vimetakiwa kuzingatia hili
Wamiliki wa vyuo binafsi vya kada ya famasi nchini wametakiwa wasibadilishe vyuo vikawa kama biashara kwani Serikali inatarajia kupata wataalam ambao wataweza kutoa huduma zinazostahili kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.