"Wadukuzi ni wengi mno, watakujazia Mil. 100"- JPM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kuhakikisha kwamba taarifa zinazojazwa na watumishi wa umma haziwekwi mtandaoni, kwani kufanya hivyo inaondoa usiri wa taarifa hizo na kuwapa nafasi kubwa wadukuzi.