Serikali yashangaa upandaji bei ya saruji
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha hadi kufikia tarehe 20, Novemba, 2020 wanafahamu ni kwanini bei ya saruji imepanda kutoka bei ya kawaida kwa kutembelea viwanda na mawakala wa saruji wakati serikali haijapandisha kodi.