
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
Majaliwa ametoa agizo hilo leo akiwa Ikulu ya Rais Chamwino mara baada ya kuapishwa, ambapo amemuhakikishia Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwa ameshaanza kulishughulikia suala la upandaji wa bei ya saruji.
“Wako wenzetu wachache wameanza kujisahau wakidhani serikali iko kwenye uchaguzi na tumeona kumeibuka upandaji bei wa saruji kwa gharama kubwa sana ambazo hazikubaliki na hakuna sababu ya msingi , serikali yetu mika mitano iliyopita imefanya mambo makubwa sana hatutarajii saruji kuwa na bei hiyo ambayo tumeiona” amesema Waziri Majaliwa
Aidha,kwa kukazia suala hilo, Mh. Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa kote nchini,kutembelea viwanda na mawakala wanaozalisha na kuuza saruji,“Niwaagize ma RCniwape mpaka tarehe 20, saa 4:00 asubuhi, kila mmoja aende kwenye kiwanda na mawakala wa saruji waangalie ni kwanini bei ya saruji imepanda kutoka bei ya kawaida na ongezeko la zaida ya Sh. 3000, hadi 4000 bila sababu yeyote wakati serikali haijaongeza kodi tunahitaji maelezo kwanini bei ya saruji imepanda kiasi hicho”