Viongozi wa dini watoa neno kwa walioshindwa
Baadhi ya viongozi wa kiroho mkoani Dodoma wamewashauri wagombea wa nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, na matokeo ya mshindi wa urais kutangazwa jana Oktoba 30, kuhakikisha wanaridhika na matokeo waliyoyapata na kushirikiana katika kujenga nchi.