Kigogo wa Serikali ahojiwa TAKUKURU kwa saa 2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima amehojiwa kwa takribani kwa saa 2 na dakika 55 katika ofisi za TAKUKURU - Dodoma, kuhusiana na tuhumu za viongozi wa wizara hiyo kuingia makubaliano kwa kusaini mkataba wa kununua vifaa vya zimamoto.