Wizara ya Elimu yafunguka mabadiliko ya ufaulu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zenye madai kuwa Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako ametangaza viwango vipya vya ufaulu kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na sita.