Jumatano , 28th Nov , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amekutana na Rais wa zamani Afrika Kusini na mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Afrika linalohusu udhibiti na utakatishaji fedha haramu, Thabo Mbeki ambapo walijadili masuala mbalimbali ikiwemo upambanaji fedha haramu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, na Rais wa zamani Afrika Kusini, Thabo Mbeki.

haramu barani afrika.

Akizungumza Jijini Dar es salaam Rais Magufuli amesema tatizo la upotevu wa pesa barani afrika limekuwa sugu kutoka  na baadhi ya wawekezaji kutoka mataifa yaliyo nje ya Afrika kudai wamekuwa wakiingia hasara kwenye biashara zao tofauti na uhalisia.

“Nchi za Afrika zimekuwa zikipoteza hela nyingi kwa mwaka tunapoteza zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.4 hadi dola milioni 2 na kiwango cha kupoteza fedha hizo kikiwa hela ni asilimia 9, Tanzania tumepoteza Dola za Kimarekani bilioni 19 kwa miongo minne,” amesema Rais Magufuli.

Suala la upotevu wa hela Afrika limeonekana kuwa kubwa kuliko fedha ambazo tunapewa kama msaada, wengine wanakuja kama wawekezaji lakini wanakuwa wanapandisha gharama kwenye baadhi ya miradi ambayo wanawekeza,”

Kuna hela nyingine zinakuja zinamwagwa kama hela za ubadhirifu ili ziingie kwenye mzunguko wa fedha zetu” ameongeza Rais Magufuli.

Mapema leo hii Ikulu Jijini Dar es salaam pia Rais Magufuli amekutana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Nicolai Astrup ambapo walijadili masuala masuaala ya uwekezaji wa gesi pamoja na masuala ya kielimu.