Hatujaombana msamaha na Jide - Mwana FA
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye hivi karibuni amemaliza tofauti zake na msanii mwenzake Lady Jaydee baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kwa muda mrefu, amesema hakuna mtu aliyemuomba msamaha mwenzake kati yao ili kuyamaliza.