Bibi na wajukuu wake wafariki kwa maji
Bibi wa miaka 63 pamoja na wajukuu zake wawili wamefariki dunia kwa kusombwa na maji ya mvua yaliyobomoa nyumba yao katika mtaa wa Bomani wilayani Tarime mkoani Mara, baada ya mto kufurika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.