Manula atoa kauli kuhusu kusaini Simba
Kipa Bora wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara msimu huu na nyota wa Azam FC, Aishi Manula, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kufuatia taarifa zinazoenezwa kuwa tayari amesaini Simba kwa ajili ya kuitumikia kwa msimu ujao.

