Mwili wa Mama Lucy Kibaki wapokelewa Kenya
Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret wamewaongoza baadhi ya wananchi wa Kenya kuupokea mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya, Mama Lucy Kibaki uliowasili leo alfajiri Jijini Nairobi.
Mwili wa Mama Lucy Kibaki, umewasili leo majira ya saa kumi na na moja alfajiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ukiwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Kenya, iliyotokea Jijini London, Uingereza.