Jumapili , 1st Mei , 2016

Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret wamewaongoza baadhi ya wananchi wa Kenya kuupokea mwili wa

Wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mama Lucy Kibaki

Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret wamewaongoza baadhi ya wananchi wa Kenya kuupokea mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya, Mama Lucy Kibaki uliowasili leo alfajiri Jijini Nairobi.

Mwili wa Mama Lucy Kibaki, umewasili leo majira ya saa kumi na na moja alfajiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ukiwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Kenya, iliyotokea Jijini London, Uingereza.

Ndege hiyo iliyoubeba mwili wa Mama Lucy Kibaki, alikuwemo pia rais mstaafu Mwai Kibaki, familia yake na marafiki wa karibu waliokuwa na Mama Kibaki Jijini London kwa matibabu kabla ya kufariki dunia siku ya jumanne.