Barcelona yafikia rekodi ya Real Madrid
Mabao ya Lionel Messi na Gerard Piqué yameiwezesha Barcelona kutoka nyuma na kuifunga Sevilla 2-1 Uwanjani Camp Nou na kuifikia Rekodi iliyowekwa na Real Madrid ya kucheza mitanange 34 bila kupoteza hata moja katika Mashindano yote.