Wachezaji wa Barcelona Jord Alba(kushoto)Lionel Messi (kati)na Neymar(kulia)wakishangila bao la kusawazisha jana dhidi ya Sevilla mechi waliyofanikiwa kushinda bao 2-1.
Real Madrid ilifanikiwa kufanya hivyo msimu wa mwaka 1988/89 na sasa Barcelona wamekwenda pia michezo 34 bila kufungwa tangu wachapwe bao 2-1 na Sevilla Estadio Ramon Sanchez Pizjuan Mwezi Oktoba Mwaka Jana huku wakishinda mechi 27 kati ya hizo katika Mashindano yote.
Wacatalunya hao ambao kwa sasa wanaalama 66 wanawania kuandika rekodi mpya Alhamisi usiku watakapoumana na Rayo Vallecano kwenye La Liga.
Kwenye mechi ya jana Sevilla walitangulia kufunga kwa bao la dakika ya 20 la Victor Perez Vitolo lakini Lionel Messi akasawazisha Dakika ya 31 na Dakika ya 48 kumpasia Gerard Pique aliyefunga bao la pili na kuketi kileleni kwa tofauti ya pointi 8 na Atletico Madrid..