Rais Samia afanya uteuzi mpya
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt Hashil Abdallah kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara . Kabla ya uteuzi huo Dkt Abdallah alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Uwekezaji).