Diwani na wenzake mahakamani kwa tuhuma za mauaji
Watu 14 akiwemo Diwani wa Kata ya Buzilasoga David Shilinde, Mwenyekiti wa CCM Kijiji cha Ikoni B William Nengo na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Tiluloza Alphonce, wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aitwaye Getruda Dotto.