Wakamatwa kwa kuua Pundamilia na Digidigi
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wakazi wanne wa wilayani Mwanga kwa tuhuma za kufanya ujangili ambapo wanadaiwa kuwauwa kwa kuwapiga risasi na kuwacharanga mapanga Pundamilia watatu na digidigi mmoja.