"Serikali haitapunguza eneo la Msitu Mbiwe" - Mary
Serikali imesema haitapunguza eneo la Hifadhi ya Msitu wa Mbiwe kwa ajili ya matumizi ya wananchi na shughuli za kiuchumi, ikieleza kuwa itaendelea kulihifadhi eneo hilo kwa lengo la kulinda bioanuai zilizopo katika msitu huo.