Ashambuliwa na kujeruhiwa akitoka harusini
Baraka Mayala (24) mkazi wa Kitongoji cha Burugalila Kijiji cha Bujinge Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga ameshambuliwa na watu wasiojulikana na kumjeruhi vibaya maeneo mbalimbali ya mwili wake wakati akitoka kwenye harusi akielekea nyumbani majira ya saa nne usiku.