Mwanafunzi aliyeuawa na 'Panya road' kuzikwa Dar
Mwili wa Maria Baso (24) mwanachuo aliyeuawa na kikundi cha wahalifu wanaodhaniwa kuwa 'Panya road' usiku wa kuamkia Septemba 14,2022, unatarajiwa kuzikwa jumamosi ya Septemba 17, 2022 Mwenge jijini Dar es Salaam, huku wazazi wakiendelea kuomba vyombo usalama kukomesha vitendo hivyo.