Chai na vitafunwa vya viongozi kukatwa
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemuagiza mlipaji Mkuu wa Serikali kukaa na maafisa masuuli wote ili kuyaangalia upya mafungu ya matumizi mengineyo ndani ya serikali ili miradi yote ya maendeleo isiathirike, ikiwemo kukata kwenye chai na vitafunwa vya viongozi.