Mhandisi akaa ofisini miaka minne bure
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, katikati ya mkutano na wananchi wa Kondoa Vijijini aliwaagiza polisi kumkamata na kumweka rumande Meneja wa RUWASA wa wilaya hiyo Mhandisi Falaura Kikusa, mara baada ya kubainika kushindwa kutekeleza mradi wowote tangu aingie ofisini kwa kipindi cha miaka minne.