Mwanamke auawa na mamba akichota maji
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Orester Haule (25) mkazi wa kijiji cha Kipingu Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe amefariki dunia baada ya kukamatwa na mamba na kumzamisha kwenye Maji wakati akichota maji katika mto Ruhuhu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani