
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba
Hayoyamebainishwa hii leo Septemba 20, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, na kusema punguza la tozo hizo litaanza kutumika Oktoba Mosi mwaka huu.
"Marekebisho yanayotarajiwa kufanyika ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande zote, kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na ile ya kwenda benki moja kwenda nyingine, kutowahusisha wafanyabishara kama ilivyokuwa kwenye kanuni za sasa, kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia ATM," amesema Waziri wa fedha