Watu sita wafariki kwenye ajali Manyara
Jumla ya watu 6 wamepoteza maisha na wengine 20 kulazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, kufuatia ajali ya basi lililoanguka katika kijiji cha Chekanao, huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa mwendokasi wa dereva.

