Panya road wanaodaiwa kumuua Maria wauawa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam liliwajeruhi na baadaye kufariki dunia, watu sita wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha maarufu kama panya road eneo la Makongo, ambapo wawili kati yao wanadaiwa kuhusika na mauaji ya Maria Basso aliyeuawa Kawe.
