Mtu mmoja akutwa na viungo vya binadamu Kigoma
Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Taimu Kaogoma mkazi wa Kijiji cha Gwanupu wilayani Kakonko mkoani humo kwa Tuhuma za kukutwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu ikiwemo fuvu la kichwa na mfupa wa taya.