Jumatano , 21st Sep , 2022

Adhabu ya kifo imefutwa nchini Equatorial Guinea, ikiwa ni kwa mujibu wa sheria iliyotiliwa saini na Rais wan chi hiyo  Teodoro Obiang.

Mara ya mwisho adhabu hiyo kutekelezwa nchini humo  ilikua miaka 8 iliyopita.

Makamu wa Rais wa nchi hiyo ambaye pia ni mtoto wa kiume Rais  Obiang, Bw.Nguema Obiang Mangue amesema kwamba jambo hilo ni la kihistoria nchini humo .Kifungu kipya cha sheria cha adhabu mbadala kitafanyiwa kazi ndani ya siku 90 zijazo. 

Suala hilo limekuja ikiwa ni miaka 3 imepita tangu Rais Obiang kuahidi kukomesha adhabu hiyo. Umoja wa mataifa umepongeza hatua hiyo ambapo kwa mujibu wa kamishina wa haki za binadamu wa UN , Nada Al-Nashif amesema kwamba "ninaikaribisha hatua hii mpya ya Equatorial Guinea kufuta adhabu ya kifo ambayo inaendana kiyume na haki zabinadamu’’ 

Adhabu ya kifo bado inatumika katika nchi  zaidi ya 30 za bara la Afrika , lakini nchi 20 kati ya hizo hazijatekeleza adhabu hiyo kwa miaka zaidi ya 10 sasa