Kipato duni chavunja zaidi ya ndoa 300 Dar
Zaidi ya ndoa 365 zimevunjika katika Manispaa ya Temeke katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi sasa. Hayo yamebainishwa na Afisa ustawi wa Jamii wa manispaa hiyo Lilian Mafole na kusema chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hizo ni mifarakano, wivu wa mapenzi na kipato duni.