Urusi na Ukraine kufungua usafirishaji wa nafaka
Urusi na Ukraine leo zinatarajiwa kutia saini mkataba wa kufungua tena shughuli za usafirishaji nafaka kupitia bandari za Ukraine zilizopo kwenye mwambao wa bahari nyeusi, hatua itakayofungua njia ya kupunguza mzozo wa upungufu wa chakula duniani.